Yusuf 12:68
يوسفوَلَمَّا دَخَلُوا۟ مِنْ حَيْثُ أَمَرَهُمْ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغْنِى عَنْهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ إِلَّا حَاجَةً فِى نَفْسِ يَعْقُوبَ قَضَىٰهَا ۚ وَإِنَّهُۥ لَذُو عِلْمٍ لِّمَا عَلَّمْنَـٰهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Na walipoingilia pale alipowaamrisha baba yao, hakuwa wa kuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni haja tu iliyokuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliyoitimiza. Na hakika yeye alikuwa na elimu kwa sababu tulimfundisha, lakini wengi wa watu hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo ingia kama alivyo waamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, isipo kuwa ni haja tu iliyo kuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliitimiza. Na hakika yeye alikuwa na ilimu kwa sababu tulimfundisha; lakini watu wengi hawajui. [68]
[68] Wale vijana wakapokea wasia wa baba yao, wakapitia milango mbali mbali. Wala hayo si kama ndiyo ya kuwazuilia madhara walio kwisha andikiwa na Mwenyezi Mungu! Na Yaa'qub akijua hayo, kwani yeye alikuwa na ilimu tuliyo mfundisha. Lakini wasia wake ulikuwa ni kwa haja aliyo kuwa nayo nafsini mwake tu, nayo ni huruma ya baba kwa wanawe ambayo ameidhihirisha katika huu wasia. Na hakika watu wengi hawana ujuzi kama alio kuwa nao Yaa'qub wakamwachia mambo yao Mwenyezi Mungu awalinde.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walipoingia kupitia milango mbalimbali, kama alivyowaamrisha baba yao, hilo halikuwa ni lenye kuwazuilia uamuzi wa Allah Mtukufu kwao, isipokuwa ilikuwa ni huruma ndani ya moyo wa Ya‛qûb juu yao wasipatikane na jicho la husuda. Na Ya‛qûb ni mwenye ujuzi mkubwa wa mambo ya Dini yake aliyofundishwa na Allah Mtukufu kwa njia ya wahyi, lakini wengi wa watu hawajui mwisho wa mambo na undani wake, na pia hawayajui anayoyajua Ya‛qûb, amani imshukie, katika mambo ya dini yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net