Yusuf 12:67
يوسفوَقَالَ يَـٰبَنِىَّ لَا تَدْخُلُوا۟ مِنۢ بَابٍ وَٰحِدٍ وَٱدْخُلُوا۟ مِنْ أَبْوَٰبٍ مُّتَفَرِّقَةٍ ۖ وَمَآ أُغْنِى عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۖ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَعَلَيْهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُتَوَكِّلُونَ
Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kwa kupitia milango tofautitofauti. Wala mimi siwafai kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake mimi nimetegemea, na juu yake na wategemee wanaotegemea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni kwa milango mbali mbali. Wala mimi sikufaeni kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye wategemee wanao tegemea. [67]
[67] Yaa'qub alitua kwa ahadi ya watoto wake. Kisha huruma ilimpelekea kuwausia kuwa watapo ingia Misri waingie kupita milango mbali mbali, ili watu wasiwapige kijicho, huenda wakadhurika. Akasema: Wala mimi sina uwezo wa kukulindeni na madhara. Kwani mwenye kuzuia madhara ni Mwenyezi Mungu tu, na hukumu ni yake Yeye pekee. Mimi nimemtegemea Yeye, na mambo yangu na yenu yote nimemwachia Yeye. Na juu yake Yeye peke yake wategemee wote wanao tegemeza mambo yao, kwa kumuamini Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na akasema baba Yao kuwaambia wao, Enyi wanangu mtakapoingia nchi ya Misri, msiingie kwa mlango mmoja, lakini ingieni kwa milango mbalimbali, ili msipatwe na jicho la husuda. Na mimi nikiwapa wasia huu, siwakingi na chochote Alichokiamua Allah Mtukufu kwenu. Hakuna uamuzi wowote isipokuwa ni ule wa Allah Mtukufu Peke Yake, Kwake Yeye nimetegemea na nimeamini, na juu Yake Peke Yake waumini wanategemea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net