Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 66

Yusuf 12:66

يوسف

قَالَ لَنْ أُرْسِلَهُۥ مَعَكُمْ حَتَّىٰ تُؤْتُونِ مَوْثِقًا مِّنَ ٱللَّهِ لَتَأْتُنَّنِى بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يُحَاطَ بِكُمْ ۖ فَلَمَّآ ءَاتَوْهُ مَوْثِقَهُمْ قَالَ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ

Maana

Akasema: Sitamuachilia pamoja nanyi mpaka mnipe agano kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtanijia naye isipokuwa ikiwa mtazungukwa. Basi walipompa agano lao, alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Sitampeleka nanyi mpaka mnipe ahadi kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima mtamrejeza kwangu, ila ikiwa mmezungukwa. Basi walipo mpa ahadi yao alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo. [66]

[66] Waliweza wana wa Yaa'qub kumkinaisha baba yao, na maneno yao yakampata palipo. Akaacha kushikilia kumzuia mwanawe asende Misri na nduguze. Lakini moyo wake haukuwacha kuwa na haja ya kuzidi kutuzwa. Kwa hivyo aliwaambia: Sitomwacha ende nanyi ila baada ya kunipa dhamana ya nguvu. Niahidini kwa Mwenyezi Mungu kwamba mtanirudishia mtapo rudi. Na wala msiache kumrudisha ila mkiangamia nyinyi au ikawa adui amekuzungukeni akakushindeni. Wakamkubalia na wakampa ahadi aliyo itaka. Na hapo tena akamshuhudisha Mwenyezi Mungu ahadi yao na viapo vyao kwa kusema: Mwenyezi Mungu anayashuhudia na kuyaona yote haya yanayo pita baina yetu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ya‛qûb, amani imshukie, akasema kuwaambia, Sitamuacha aende na nyinyi mpaka mchukue ahadi na mniapie kwa Allah Mtukufu kwamba mtamrudisha kwangu, isipokuwa iwapo mtashindwa nguvu msiweze kumuokoa. Basi walipompa ahadi ya Allah Mtukufu kwa lile alilolitaka, Ya‛qûb alisema, «Allah Mtukufu kwa tunalolinena Ndiye mtegemewa» Yaani, ushahidi Wake kwetu na utunzi Wake zinatutosha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net