Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 65

Yusuf 12:65

يوسف

وَلَمَّا فَتَحُوا۟ مَتَـٰعَهُمْ وَجَدُوا۟ بِضَـٰعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ قَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَا مَا نَبْغِى ۖ هَـٰذِهِۦ بِضَـٰعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ كَيْلٌ يَسِيرٌ

Maana

Na walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi hapa bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda kaka yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walipo fungua mizigo yao wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo. [65]

[65] Na wale nduguze Yusuf hawakujua kuwa Yusuf aliwatilia bidhaa zao katika mizigo yao. Walipo ifungua wakakuta mali yao, na wakaona hisani aliyo wafanyia Yusuf, wakaitumia hiyo kuzidi kumpoza moyo Yaa'qub, na kumkinaisha awakubalie kwa aliyo yataka Mheshimiwa. Wakazidi kumshikilia akubali, wakamkumbusha makhusiano yao yalio wafunga kwa baba mmoja. Wakasema: Ewe baba yetu! Unataka wema gani zaidi kuliko haya, na hayo yatayo kuwa? Haya mali yetu tumerudishiwa bila ya kuchukuliwa chochote. Basi natusafiri na ndugu yetu, na tuwaletee watu wetu mahitaji, nasi tutamchunga ndugu yetu, na tutaongeza mahitaji shehena ya ngamia kuwa ni haki ya ndugu yetu! Kwani yule Mheshimiwa kapanga kuwa kila mtu humpa shehena ya ngamia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walipofungua vyombo vyao walipata kwamba thamani ya bidhaa waliyoitoa wamerudishiwa. Wakasema, «Ewe baba yetu! Tuombe nini zaidi ya hii? Hii ni thamani ya bidhaa zetu, Kiongozi ameturudishia, basi kuwa na utulivu kuhusu ndugu yetu na muache aende na sisi ili tupate kuwaletea watu wetu chakula kingi, tumtunze ndugu yetu na tupate kuongeza twesha ya ngamia kwa ajili yake. Kwani Kiongozi anampimia kila mtu twesha ya ngamia mmoja; na hilo ni jambo jepesi kwake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net