Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 64

Yusuf 12:64

يوسف

قَالَ هَلْ ءَامَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمْ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَٱللَّهُ خَيْرٌ حَـٰفِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Maana

Akasema: Je, niwaamini juu yake isipokuwa kama nilivyowaamini kwa kakaye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi wa kulinda, naye ndiye Mbora zaidi wa wanaorehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote. [64]

[64] Yaa'qub yalimtibuka moyoni mwake yale ya zamani, akayaunganisha na haya mapya. Akawaambia wanawe: Nikikukubalieni itakuwa hali yangu ni ya ajabu; kwani nikikuaminini kwa huyu ndugu yenu haitakuwa ila mfano wa pale nilipo kuaminini kwa Yusuf. Mkamchukua kisha mkarudi mkisema: Kaliwa na mbwa mwitu! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye anaye nitosheleza katika kumlinda mwanangu. Wala mimi simtegemei mtu ila Yeye, kwani Yeye ndiye Mlinzi aliye na nguvu kuliko wote, na rehema yake ni kunjufu mno, hatonipa tena machungu ya ndugu yake baada ya yale ya Yusuf.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Baba yao akawaambia, «Vipi nitawaamini juu ya Binyãmîn, na nilishawaamini juu ya Yûsuf kabla yake, mkaahidi kumhifadhi na msilitekeleze hilo? Mimi siziamini ahadi zenu na utunzi wenu, lakini mimi nauamini utunzi wa Allah Mtukufu, Bora wa wenye kutunza na Mwenye huruma zaidi kuliko wenye huruma. Namtarajia Anirehemu, Amtunze na Amrudishe kwangu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net