Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 63

Yusuf 12:63

يوسف

فَلَمَّا رَجَعُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَبِيهِمْ قَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلْكَيْلُ فَأَرْسِلْ مَعَنَآ أَخَانَا نَكْتَلْ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَـٰفِظُونَ

Maana

Basi waliporejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi. Basi muachilie ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa. Nasi hakika tutamlinda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi walipo rejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi, basi mpeleke nasi ndugu yetu ili tupate kupimiwa; na yakini sisi tutamlinda. [63]

[63] Walipo rejea kwa baba yao walimsimulia kisa chao na Mheshimiwa wa Misri, na upole wake kwao, na kwamba amewaonya kuwa atawanyima kuwapimia chakula baadae ikiwa hatokuwa nao Bin-yamini; na kwamba amewaahidi kuwatimizia kipimo na atawatukuza pindi wakirudi na ndugu yao. Wakamwambia baba yao: Mwache ende nasi ndugu yetu, kwani ukimpeleka yeye tutapimiwa chakula cha kutosha tunacho kihitajia. Nasi tunakuahidi ahadi ya nguvu ya kwamba tutafanya juhudi kumlinda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waliporejea kwa baba yao walimsimulia yaliyokuwa ya ukarimu aliowafanyia huyo kiongozi, na wakasema, «Yeye hatatupatia kitu mbeleni isipokuwa iwapo ndugu yetu ambaye tulimuelezea kuhusu yeye atakuwa na sisi. Basi tuachie tuende na yeye tutaleta chakula kingi, na tunakuahidi kwamba tutamtunza».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net