Yusuf 12:62
يوسفوَقَالَ لِفِتْيَـٰنِهِ ٱجْعَلُوا۟ بِضَـٰعَتَهُمْ فِى رِحَالِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَعْرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakaporudi kwa watu wao ili wapate kurejea tena.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakapo rudi kwa watu wao wapate kurejea tena. [62]
[62] Walipo taka kuondoka aliwaambia wafwasi wake: Watilieni thamani ya bidhaa yao waliyo kuja nayo humo humo pamoja na mizigo yao, ili waione watakapo rudi kwa watu wao, wapate kurejea tena kwa kutumai kupewa chakula kwa kuamini kuwa tunatimiza ahadi, na wawe na imani ya usalama wa ndugu yao, na baba yao azidi kutua nafsi yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf aliwaambia watumishi wake, «Ichukueni thamani ya vitu vyao muiweke kwenye vyombo vyao kwa siri, kwa matarajio wapate kuiona watakapofika kwao na watambue vile sisi tulivyowakirimu ili wapate kurudi wakiwa na matumaini ya kupata vipewa vyetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net