Yusuf 12:58
يوسفوَجَآءَ إِخْوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَعَرَفَهُمْ وَهُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ
Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia alimokuwa. Yeye akawajua, na wao hawakumjua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua. [58]
[58] Ukame ukazidi kushtadi katika nchi jirani na Misri. Ikawapata watu wa Yaa'qub shida vile vile kama ilivyo wapata wengineo. Watu walikwenda Misri kutoka kila pande baada ya kujua matengenezo ya Yusuf ya kuweka akiba chakula, na kujitayarisha kwake kwa miaka ya ukame. Yaa'qub aliwatuma wanawe wende kutafuta chakula, lakini akabaki naye nduguye Yusuf kwa mama kwa kumkhofia. Wale watoto wake walipo fika Misri wakenda moja kwa moja kwa Yusuf, naye akawatambua, lakini wao hawakumjua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nduguze Yûsuf walifika Misri, baada ya kushukiwa na ukame katika nchi yao, ili wachukue chakula kutoka huko. Wakaingia kwake na yeye, kwa nguvu ya akili yake ya kutambua na werevu wake, akawajua na wao wasimjue kwa muda mrefu uliopita na kwa kubadilika umbo lake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net