Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 59

Yusuf 12:59

يوسف

وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ قَالَ ٱئْتُونِى بِأَخٍ لَّكُم مِّنْ أَبِيكُمْ ۚ أَلَا تَرَوْنَ أَنِّىٓ أُوفِى ٱلْكَيْلَ وَأَنَا۠ خَيْرُ ٱلْمُنزِلِينَ

Maana

Na alipowatengenezea tayari haja yao, alisema: Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi hakika ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wanaokaribisha?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo watengenezea tayari haja yao alisema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba. Je! Hamwoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa kukirimu? [59]

[59] Yusuf akaamrisha wakaribishwe ugeni, na wapewe mahitaji wanayo yataka. Wakapewa hayo. Akaingia kuzungumza nao na kuwauliza hali zao kama mtu asiye wajua! Naye anawajua vyema. Nao wakamwambia kuwa wamemwacha ndugu yao mmoja kwa baba yao, kwani hapendi kuachana naye. Naye huyo ni Bin-yamini nduguye Yusuf kwa baba na mama. Basi yeye akasema: Mwacheni ndugu yenu aje nanyi, wala msiogope chochote. Nyinyi mmekwisha ona vipi ninavyo kutimizieni vipimo vyenu, na ninavyo kukirimuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yûsuf aliamuru wakirimiwe na wakaribishwe vizuri, kisha akawapa chakula walichotaka. Na walikuwa wamemwambia kwamba wana ndugu yao wa kwa baba ambaye hawakumleta pamoja nao, wakimaanisha ndugu yake Binyãmîn, akasema, «Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba, kwani hamuoni kwamba mimi nimewapimia chakula vizuri na nimewakirimu kwa kuwakaribisha, na mimi ni mwema wa kuwakaribisha?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net