Yusuf 12:57
يوسفوَلَأَجْرُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَكَانُوا۟ يَتَّقُونَ
Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa walio amini na wakawa wachamungu. [57]
[57] Na malipo yao ya Akhera ni bora zaidi na yanalingana zaidi na hao wanao msadiki Yeye na Mitume wake, na ikawa wanaingojea Siku ya Hisabu na wanaikhofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika malipo mema ya Akhera ni makubwa zaidi kuliko malipo ya duniani kwa wenye Imani na uchamungu ambao wanayaogopa mateso ya Allah Mtukufu na wanamtii Yeye katika maamrisho Yake na makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net