Yusuf 12:56
يوسفوَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِى ٱلْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَآءُ ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَن نَّشَآءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Basi hivyo ndivyo tulivyomuimarisha Yusuf katika ardhi, akawa anakaa humo popote anapotaka. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo popote anapo penda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo ya wafanyao mema. [56]
[56] Mfalme alilikubali ombi lake, akamfanya waziri wake. Hivyo basi Mwenyezi Mungu alimneemesha Yusuf kwa neema nzuri, akampa madaraka na uwezo katika nchi ya Misri, akienda humo atakapo. Na hii ndiyo shani yake Mwenyezi Mungu kwa waja wake, humpa neema yake amtakaye katika wao, wala hawanyimi thawabu zao, bali huwapa ujira wao wa wema wautendao kwa kuwalipa mema hapa hapa duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama Allah Mtukufu Alivyomneemesha Yûsuf kwa kumtoa jela, Alimmakinisha katika nchi ya Misri akawa ashukia popote pale anapotaka. Allah Mtukufu Anampa rehema Zake Anayemtaka kati ya waja wake wachamungu, na Hayapotezi malipo ya yoyote aliyefanya matendo mema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net