Yusuf 12:55
يوسفقَالَ ٱجْعَلْنِى عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلْأَرْضِ ۖ إِنِّى حَفِيظٌ عَلِيمٌ
Yusuf akasema: Nifanye msimamizi wa hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yusuf akasema: Nifanye mshika khazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mjuzi. [55]
[55] Mfalme akajua kwake Yusuf kuwa yeye ni muangalizi mwema na mweza wa kazi yake. Na Yusuf akahisi hayo. Hapo akataka amfanye waziri akamwambia: Nitawalishe juu ya khazina zote za mamlaka yako, na ghala za nchi yako. Kwani mimi kama ulivyo yakinika mwenyewe naweza kuendesha mambo ya serikali, nami ni mlinzi, na najua kupanga na kuendesha mambo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf akataka kuwanufaisha waja na kueneza uadilifu baina yao, alimwambia mfalme, «Nifanye mimi kuwa msimamizi wa hazina za Misri, kwani mimi ni mshika hazina mwaminifu mwenye ujuzi na busara juu ya vitu ninavyosimamia».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net