Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 54

Yusuf 12:54

يوسف

وَقَالَ ٱلْمَلِكُ ٱئْتُونِى بِهِۦٓ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِى ۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلْيَوْمَ لَدَيْنَا مَكِينٌ أَمِينٌ

Maana

Basi mfalme akasema, "Nijieni naye, awe wangu mwenyewe hasa." Basi alipomsemesha, akasema, "Hakika wewe leo umekwishakuwa imara kwetu na umeaminika."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa. Basi alipo msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika. [54]

[54] Usafi wa Yusuf ulipo dhihiri kwa mfalme, aliazimu amwite. Akawatuma watu wake wamlete awe wake yeye mwenyewe wa kumsafia niya. Basi alipo hudhuria na yakapita baina yao mazungumzo, mfalme akaathirika na utukufu wa Yusuf kwa usafi wa nafsi yake, na ubora wa rai zake! Akamwambia: Sasa wewe kwangu utakuwa na cheo cha hishima kilicho thibiti. Na wewe ni muaminifu kwangu ninaye kuamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mfalme, mtawala wa Misri, ilipomfikia habari kwamba Yûsuf hana hatia, alisema, «Mleteni kwangu nipate kumfanya ni miongoni mwa marafiki wangu wa kikweli na washauri wangu.» Yûsuf alipokuja, na mfalme akasema na yeye, akajua kwamba yeye hana hatia na kwamba ni mwaminifu sana na ni mwenye tabia njema, alimwambia, «Wewe leo hapa kwetu una heshima kubwa na unaaminiwa kwa kila kitu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net