Yusuf 12:53
يوسفوَمَآ أُبَرِّئُ نَفْسِىٓ ۚ إِنَّ ٱلنَّفْسَ لَأَمَّارَةٌۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّىٓ ۚ إِنَّ رَبِّى غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Nami sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya, isipokuwa kile alichorehemu Mola wangu Mlezi. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NAmi sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipo kuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. [53]
[53] Wala sidai kuwa nafsi yangu haitelezi; kwani ni tabia ya nafsi kumili kwenye matamanio, na kupendelea maovu na shari. Isipo kuwa nafsi aliyo ilinda Mwenyezi Mungu na akaiweka mbali na maovu. Na hakika mimi ninatumai rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha wake, kwani Yeye ni Mkunjufu wa kusamehe dhambi za wenye kutubu, na yu karibu wa kuwarehemu waja wake walio kosa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema mke wa kiongozi, «Sijisafishi nafsi yangu, kwani nafsi inamwamrisha mtu sana kufanya maasia, kwa kutaka kupata utamu wa inavyopenda, isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Amemhifadhi. Kwani Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za waliotubia miongoni mwa waja Wake, ni Mwenye huruma nao sana».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net