Yusuf 12:52
يوسفذَٰلِكَ لِيَعْلَمَ أَنِّى لَمْ أَخُنْهُ بِٱلْغَيْبِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى كَيْدَ ٱلْخَآئِنِينَ
Hayo ni ili ajue ya kwamba sikumfanyia hiyana alipokuwa hayupo, na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi njama za wahaini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni apate kujua ya kwamba mimi sikumfanyia khiyana nyuma yake; na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi hila za makhaini. [52]
[52] Haya mimi naungama kwa kweli ninayo itoa, apate kuwa na yakini Yusuf kuwa mimi sikuchukua fursa ya kuto kuwepo alipo kuwa gerezani nikaendelea na khiyana, na nikamdhulumu kwa kumtuhumu. Na kwa kuwa hakika Mwenyezi Mungu haijaalii kufanikiwa mipango ya makhaini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Neno hilo nililolisema la kumwepushia Yûsuf tuhuma na kujikubalia makosa mimi mwenyewe ni kwa ajili mume wangu ajue kwamba mimi sikumfanyia hiana kwa kumzulia urongo na hayakutokea machafu kutoka kwangu pamoja na kuwa nilimtaka Yûsuf. Nimekubali hilo ili kuonyesha wazi kuwa mimi sina hatia wala yeye hana hatia na kwamba Allah Mtukufu Hawaafikii wala Hawaongozi wenye kufanya hiana katika uhaini wao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net