Yusuf 12:51
يوسفقَالَ مَا خَطْبُكُنَّ إِذْ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفْسِهِۦ ۚ قُلْنَ حَـٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِن سُوٓءٍ ۚ قَالَتِ ٱمْرَأَتُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْـَٔـٰنَ حَصْحَصَ ٱلْحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفْسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipomtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi (Mwenyezi Mungu apishe mbali)! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa yule akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliyemtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipo mtaka Yusuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliye mtaka kinyume na nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli. [51]
[51] Mfalme akawakusanya wale wanawake, na akawauliza: Ilikuwa vipi hali yenu pale mlipo jaribu kumkhadaa Yusuf aghafilike na wema wake na usafi wa nafsi yake? Je, mlimwona amemili kwenu? Wakamjibu: Mwenyezi Mungu ametakasika! Hakumsahau mja wake hata uchafuke usafi wake. Sisi hatukuona kwake lolote la kumtia dosari. Hapo basi wema ukapata nguvu katika moyo wa Zuleikha (mke wa Mheshimiwa) akaingia kusema: Sasa kweli imedhihiri! Ni mimi ndiye niliye mkhadaa, na nikajaribu kumzaini kinyume na nafsi yake kwa kumghuri. Lakini yeye alishikilia usafi wake! Na sasa nahakikisha kuwa yeye ni katika watu wa kweli. Na ni haki tupu alipo nirudishia tuhuma mimi na kunitia makosani!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfalme akasema kuwaambia wanawake walioijeruhi mikono yao. «Habari zenu ni zipi, mlipomtaka Yûsuf siku ya makaribisho? Kwani mliona chochote kutoka kwake chenye kutia shaka?» Wakasema, «Allah Mtukufu Atulinde! Hatujui chochote hata kidogo cha kumtia ila.» Hapo alisema mke wa Kiongozi, «Sasa umefunuka ukweli baada ya kufichika. Mimi ndiye niliyejaribu kumtia hatiani kwa kumbembeleza, na akakataa. Na yeye ni katika wakweli katika kila alilolisema».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net