Yusuf 12:50
يوسفوَقَالَ ٱلْمَلِكُ ٱئْتُونِى بِهِۦ ۖ فَلَمَّا جَآءَهُ ٱلرَّسُولُ قَالَ ٱرْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَسْـَٔلْهُ مَا بَالُ ٱلنِّسْوَةِ ٱلَّـٰتِى قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّى بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ
Na mfalme akasema: "Nijieni naye!" Basi mjumbe huyo alipomjia, Yusuf akasema: Rudi kwa bwana wako na umuulize wana nini wale wanawake waliojikatakata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema njama zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mfalme akasema: Mleteni kwangu! Basi mjumbe alipo mjia Yusuf alisema: Rejea kwa bwana wako ukamuulize khabari ya wale wanawake walio jikata mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao. [50]
[50] Mfalme akamwona Yusuf atakuwa na faida naye kwa ule uwezo wake kuifasiri ndoto yake, na akaazimia amwite. Akawaamrisha wasaidizi wake wamlete. Alipo mfikia mjumbe akamwabia kuwa mfalme anamtaka, khabari hiyo haikumpapatisha, juu ya kuwa ina bishara ya kufunguliwa kwake. Wala kule kutamani kutoka kwa mfungwa kwenye dhiki za jela na taabu zake hakukuitikisa subira yake. Akakhiari angoje mpaka idhihirike kuwa hana makosa kuliko kufanya haraka kutoka na huku yale aliyo tuhumiwa bado yamemganda. Akamwambia mjumbe: Rejea kwa bwana wako umtake ayaangalie tena yale mashtaka niliyo shitakiwa, awaulize wale wanawake walio kusanywa na mke wa Mheshimiwa kwa kunifanyia hila mimi, wakababaika na wakajikata mikono yao: Je! Walipo toka kwenye yale majaribio walikuwa wanaamini kuwa mimi sina makosa na safi, au waliniona ni mchafu na mzinifu? Mimi nataka haya ipate kuonekana hakika katika macho ya watu. Ama Mola wangu Mlezi anavijua vyema vitimbi vyao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfalme akasema kuwaambia wasaidizi wake, «Mtoeni jela huyo mtu aliyefasiri ndoto, na mleteni kwangu.» Yule aliyetumwa na mfalme alipomjia (Yûsuf) kumwita. Yûsuf alisema kumwambia, «Rudi kwa bwanako mfalme umtake awaulize wanawake walioijeruhi mikono yao juu ya uhakika wa mambo yao na habari zao na mimi, ili ukweli ufunuke kwa wote, na kutokuwa na hatia kwangu kuwe wazi, kwani Mola wangu ni Mjuzi zaidi wa mambo waliyoyapanga na waliyoyafanya, hakuna chochote kinachofichika Kwake katika hayo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net