Yusuf 12:49
يوسفثُمَّ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao ndani yake watu watasaidiwa na watakamua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na watakamua. [49]
[49] Kisha baada ya miaka hiyo ya ukame utakuja mwaka watu watasaidiwa kwa mvua, na watakamua zabibu na zaituni, na kila cha kukamuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Kisha utakuja, baada ya miaka hii ya ukame, mwaka ambapo watu watanyeshezewa mvua, na hivyo basi Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Awaondolee shida, hapo wakamue matunda kwa wingi wa mavuno na neema».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net