Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 48

Yusuf 12:48

يوسف

ثُمَّ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ

Maana

Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayokula kile mlichoiwekea isipokuwa kidogo katika kile mtakachokihifadhi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayo kula kile mlicho iwekea isipo kuwa kidogo mtacho kihifadhi. [48]

[48] Kisha baada ya miaka hii ya neema itakuja saba ya ukame. Mtakula kile mlicho weka akiba, isipo kuwa kidogo mtacho kificha na kukihifadhi, ili kiwe mbegu ya kupandia baadae

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha itakuja, baada ya miaka ya neema, miaka yenye ukame mkali. Watu wa wakati huu watakula chakula mlichowahifadhia hapo nyuma, isipokuwa kichache mtakachokihifadhi na kukiweka akiba kiwe ni mbegu za kupandia mimea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net