Yusuf 12:47
يوسفقَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦٓ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ
Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Kwa hivyo mtakachovuna, kiwacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtachokula kwacho.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni katika mashuke yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula. [47]
[47] Yusuf akasema: Tafsiri ya ndoto hizo ni kuwa mtalima katika ardhi ngano, na shairi kwa muda wa miaka saba mfululizo kwa ukulima wa juhudi. Mtacho vuna kihifadhini, mkiache katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtacho kila katika miaka hiyo, kwa uangalizi mzuri. Aya hii inawafikiana na ilimu za kisasa kuwa kuweka punje katika mashuke yake inakuwa ni hifadhi zisiharibike kwa hali ya hewa na mengineyo, na juu ya hivyo faida yake ya chakula inabaki kwa ukamilifu zaidi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf akasema kumwambia aliyemuuliza juu ya ndoto ya mfalme. «Tafsiri ya ndoto hii ni kwamba nyinyi mtaendelea kulima kwa bidii kwa miaka saba mfululizo ili mapato yawe mengi, basi kile mtakachokivuna kila mara kiwekeni akiba na mkiache kwenye masuke yake ili kihifadhike na kuingiwa na wadudu na ili kisalie kwa kipindi kirefu zaidi, isipokuwa kiasi kidogo cha nafaka mtakachokila».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net