Yusuf 12:46
يوسفيُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِى سَبْعِ بَقَرَٰتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ لَّعَلِّىٓ أَرْجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ
Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze ni nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu wapate kujua. [46]
[46] Yule mtumishi wa kumletea mfalme ulevi akenda kwa Yusuf, akamwita: Yusuf! Ewe uipendaye kweli! Tueleze nini maana ya ndoto ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba walio konda. Na ndoto ya mashuke saba mabichi na mengine makavu? Nataraji kurejea kwa watu nami nina fatwa yako, ili nao wapate kujua maana yake, na waujue ujuzi wako na fadhila yako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipofika yule mtu kwa Yûsuf alimwambia, «Yûsuf! Ewe mkweli sana! Tufasirie ndoto ya aliyeota ng’ombe saba wanono wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na akaona masuke saba mabichi na mengine makavu. Natarajia nitarudi kwa mfalme na marafiki zake niwape tafsiri ya hiyo niliyokuuliza na ili wapate kujua cheo chako na utukufu wako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net