Yusuf 12:45
يوسفوَقَالَ ٱلَّذِى نَجَا مِنْهُمَا وَٱدَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا۠ أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِۦ فَأَرْسِلُونِ
Hapo akasema yule aliyeokoka katika wale wawili na akakumbuka baada ya muda. Mimi nitawaambia tafsiri yake. Basi nitumeni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapo akasema yule aliye okoka katika wale wawili akakumbuka baada ya muda: Mimi nitakwambieni tafsiri yake. Basi nitumeni. [45]
[45] Akasema yule mtu aliye okoka katika wawili alio kuwa nao Yusuf gerezani, na akakumbuka wasia wa Yusuf, baada ya kupita muda mrefu: Mimi nitakwambieni tafsiri ya ndoto aliyo itaja mfalme. Nipelekeni kwa huyo mwenye ilimu ya kuifasiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo akasema yule aliyeokoka na kuuawa kati ya marafiki wawili wa Yûsuf ndani ya jela, na akakumbuka habari ya Yûsuf baada ya muda kupita, «Mimi nitawapa habari ya tafsiri ya ndoto hii. Nitumeni kwa Yûsuf nipate kuwaletea tafsiri yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net