Yusuf 12:44
يوسفقَالُوٓا۟ أَضْغَـٰثُ أَحْلَـٰمٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ ٱلْأَحْلَـٰمِ بِعَـٰلِمِينَ
Wakasema: Hizi ni ndoto zilizoparaganyika, wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya ndoto hizi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Hizi ni ndoto zilizo paraganyika, wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya ndoto hizi. [44]
[44] Wakasema: Hizi ni ndoto zilizo korogeka ovyo, na wasiwasi wa kuzuka tu katika nafsi ya mtu! Na sisi si wenye kujua tafsiri ya ndoto za ovyo ovyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema, «Ndoto yako hii ni mchanganyiko wa ndoto usiokuwa na tafsiri, na sisi hatukuwa ni wenye ujuzi kufasiri ndoto namna hii».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net