Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 43

Yusuf 12:43

يوسف

وَقَالَ ٱلْمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَٰتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ ۖ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَأُ أَفْتُونِى فِى رُءْيَـٰىَ إِن كُنتُمْ لِلرُّءْيَا تَعْبُرُونَ

Maana

Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba waliokonda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Niambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Nambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto. [43]

[43] Mfalme akasema: Nimeota usingizini kuna ng'ombe saba wanene wanaliwa na wengine saba walio konda madhaifu. Na nimeota mashuke saba mabichi, na mengine saba makavu. Enyi wakuu wanazuoni na wenye maarifa! Nitoleeni fatwa ya hizi ndoto zangu, ikiwa ni kweli nyinyi mnajua tafsiri za ndoto na mnaweza kuzitolea fatwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mfalme akasema, «Mimi niliona ndotoni, katika kulala kwangu, ng’ombe saba wanono wanaliwa na ng’ombe saba walioambata kwa kukonda, na niliona visuke saba vibichi na visuke saba vikavu. Enyi mabwana na wakubwa, nipeni habari ya ndoto hii, iwapo nyinyi mnafasiri ndoto».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net