Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 42

Yusuf 12:42

يوسف

وَقَالَ لِلَّذِى ظَنَّ أَنَّهُۥ نَاجٍ مِّنْهُمَا ٱذْكُرْنِى عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَىٰهُ ٱلشَّيْطَـٰنُ ذِكْرَ رَبِّهِۦ فَلَبِثَ فِى ٱلسِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ

Maana

Na akamwambia yule aliyejua kuwa ataokoka katika wawili hao: "Nikumbuke kwa bwana wako." Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akamwambia yule aliye jua kuwa atavuka katika wale wawili: Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shet'ani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa. [42]

[42] Akamwambia yule aliye kuwa atavuka: Nitaje kwa Mfalme kwa sifa zangu, na kisa changu. Asaa huenda akanifanyia insafu akanivua na haya mateso! Shetani alimshughulisha akamsahaulisha kutaja kisa cha Yusuf kwa Mfalme. Basi Yusuf akabaki gerezani kwa miaka isiyo pungua mitatu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo Yûsuf akamwambia yule aliyemjua kuwa ataokoka kati ya wale marafiki wake wawili, «Nitaje kwa bwanako mfalme na umwelezee kwamba mimi nimedhulumiwa, nimefungwa bila hatia.» Shetani akamsahaulisha mwanamume yule kumtajia mfalme hali ya Yûsuf, na kwa hivyo akakaa Yûsuf ndani ya jela miaka kadhaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net