Yusuf 12:41
يوسفيَـٰصَـٰحِبَىِ ٱلسِّجْنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسْقِى رَبَّهُۥ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا ٱلْـَٔاخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ ٱلطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِۦ ۚ قُضِىَ ٱلْأَمْرُ ٱلَّذِى فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu, yeye atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine, yeye atasulubiwa, na ndege watakula katika kichwa chake. Imekwishakatwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mkiuliza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza. [41]
[41] Enyi wenzangu wawili wa gerezani! Hii basi ndiyo tafsiri ya ndoto zenu: Ama mmoja wenu aliye kamua zabibu katika ndoto yake, atatoka jela, na atakuwa akimnywesha mvinyo Mfalme. Na ama huyu wa pili atatundikwa msalabani, na ataachwa msalabani ndege wakimla kichwa chake. Yamekwisha timia hayo mambo kama nilivyo eleza kwa mujibu mlivyo nitaka nieleze tafsiri ya hizo ndoto!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Enyi marafiki wangu gerezani, haya chukueni tafsiri ya ndoto zenu: ama yule aliyeona kwenye ndoto yake kuwa anakamua zabibu, yeye atatoka jela na atakuwa ni mwenye kuishughulikia pombe ya mfalme. Ama mwingine aliyeota kuwa anabeba mkate juu ya kichwa chake, yeye atasulubiwa na aachwe, na ndege waje wamle kichwa chake. Limeshapitishwa jambo ambalo mlikuwa mnaliuliza na limeshamalizwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net