Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 40

Yusuf 12:40

يوسف

مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسْمَآءً سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَـٰنٍ ۚ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّآ إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Hamuabudu badala yake isipokuwa majina tu mliyowaita nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka. Lakini wengi wa watu hawajui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui. [40]

[40] Hamuabudu badala ya Mwenyezi Mungu ila majina tu mliyo yazua nyinyi na baba zenu kwa mawazo bila ya kuwepo kweli. Mwenyezi Mungu hakuwateremshia hao hoja wala ushahidi wowote! Hapana wa kuhukumu nini kinacho faa kuabudiwa na kipi hakifai ila Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimnyenyekee yeyote mwenginewe, na mumuabudu Yeye peke yake. Hiyo ndiyo Dini iliyo nzima iliyo nyooka, ambayo dalili zote na ushahidi unaelekea kwake. Lakini aghlabu ya watu hawataki uwongozi wa dalili hizi, wala hawajijui kuwa wamo katika ujinga na upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nyinyi hamuabudu chochote kisichokuwa Allah Mtukufu isipokuwa ni majina yasiyokuwa na maana yoyote, mumeyafanya ni miungu, nyinyi na baba zenu, kwa ujinga wenu na upotevu; Allah Mtukufu Hakuteremsha hoja au dalili yoyote juu ya usahihi wake. Hukumu ya haki ni ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika. Yeye Ameamrisha kwamba msimtii wala msimnyenyekee Asiyekuwa Yeye, na kwamba mumuabudu Yeye Peke Yake. Na hii ndiyo Dini iliyolingana sawa isiyokwenda kombo. Lakini wengi zaidi wa watu hawalielewi hilo, hawaujui uhakika wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net