Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 25

Yusuf 12:25

يوسف

وَٱسْتَبَقَا ٱلْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُۥ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَا ٱلْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَآءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوٓءًا إِلَّآ أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke huyo akalirarua shati lake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke huyo akasema: Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewa adhabu chungu. [25]

[25] Yusuf akakimbilia mlangoni kutaka kutoka, na yule bibi naye akapiga mbio amtangulie ili amzuie kutoka. Akaivuta kanzu yake kwa nyuma ili kumzuia, akaichana. Hapo wakapambana na mume wa yule bibi mlangoni! Yule bibi akasema kumchongea Yusuf: Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanya mkeo mambo mabaya ila atiwe gerezani, au akutishwe adhabu chungu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yûsuf alikimbilia mlangoni kutaka kutoka, na yeye (mke wa kiongozi) akafanya haraka kumshika na akamvuta nguo yake kwa nyuma ili kumzuia asitoke na akaipasua. Wakamkuta mumewe kwenye mlango, hapo akasema (mke wa Kiongozi), «Ni yapi malipo ya anayetafuta jambo baya kwa mke wako, isipokuwa ni afungwe au apewe adhabu yenye uchungu?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net