Yusuf 12:24
يوسفوَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِۦ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَآ أَن رَّءَا بُرْهَـٰنَ رَبِّهِۦ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ ٱلسُّوٓءَ وَٱلْفَحْشَآءَ ۚ إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُخْلَصِينَ
Na hakika yule mwanamke alimuazimia, na Yusuf akamuazimia lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Ilikuwa hivyo, ili tumuepushie mabaya na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walioteuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa. [24]
[24] Na yule bibi aliazimia aingiane naye, na nafsi ya Yusuf ilimvutia kwake, lau kuwa hakuiona nuru ya Mwenyezi Mungu ya haki imezagaa mbele ya macho yake. Basi hakuufuata mvutio wa nafsi, na akayashinda matamanio, na akajizuilia maasi na khiana. Akathibiti juu ya usafi na kutakasika kwake. Ndio hivi tulivyo mthibitisha Yusuf kwenye usafi na kutakasika, ili tumuepushe na uovu wa khiana na maasi ya uzinzi. Hakika yeye ni miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio itakasa dini yao kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na nafsi yake ilivutika kufanya machafu, na Yûsuf nafsi yake ilipitiwa na mawazo ya kukubali, lau si yeye kuona alama miongoni mwa alama za Mola wake zenye kumkemea kufanya yale ambayo nafsi yake ilimzungumzia. Hakika tulimuonesha hilo, ili tumuepushie baya na chafu katika mambo yake yote. Yeye ni miongoni mwa waja wetu waliosafishwa walioteuliwa kwa ujumbe na waliotakasa katika kumuabudu kwao Allah Mtukufu na kumpwekesha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net