Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 23

Yusuf 12:23

يوسف

وَرَٰوَدَتْهُ ٱلَّتِى هُوَ فِى بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلْأَبْوَٰبَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ رَبِّىٓ أَحْسَنَ مَثْوَاىَ ۖ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Maana

Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake, na akafungafunga milango. Akamwambia: "Njoo!" Yusuf akasema: Audhubillahi (ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu)! Hakika Yeye ni bwana wangu, aliniweka maskani nzuri. Hakika madhalimu hawafaulu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi. [23]

[23] Na yule bibi aliye kuwa Yusuf anakaa nyumbani kwake, naye anamjua madaraka yake, alitaka kumghuri aache mwendo wake ulio safi. Akawa anajipitisha pitisha mbele yake kuonyesha uzuri wake, na kujitamanisha kwake. Hata mwishoe akamfungia milango, na akamwambia: Njoo kwangu, nimejitoa kwako! Yusuf akasema: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu, aniepusha na hiyo shari! Na vipi nifanye uchafu huo nawe, na mumeo mheshimiwa ni bwana wangu aliye niweka bora ya makamo? Hakika hawafuzu wanao wadhulumu watu kwa udanganyifu na khiana, wakajitia wenyewe katika maasi ya uzinzi!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mke wa yule kiongozi, ambaye Yûsuf alikuwa nyumbani kwake, alimtaka Yûsuf kwa upole na kubembeleza, kwa kuwa alimpenda sana na kwa ajili ya uzuri wake, na akamfungia milango na akasema kumwambia Yûsuf, «Njoo kwangu.» Akasema, «Najilinda kwa Allah Mtukufu na najihifadhi Kwake na kujihami kutokana na hayo unayoniitia ya kumfanyia hiana bwanangu aliyeyafanya mazuri mashukio yangu na akanikirimu. Sitamhini kwa watu wake. Hakika hafaulu anayedhulumu na akafanya mambo ambayo hatakiwi kuyafanya».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net