Yusuf 12:22
يوسفوَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُۥٓ ءَاتَيْنَـٰهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Na alipofikia utu uzima wake, tukampa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na alipo fikilia utu uzima tulimpa hukumu na ilimu. Na kama hivi tunawalipa wanao tenda mema. [22]
[22] Na Yusuf alipo timia ukomo wa nguvu zake tukampa hukumu yenye kusibu, na ilimu yenye kufaa. Na kama malipo haya tuliyo mpa yeye kwa wema wake, ndio tunavyo wapa wote walio wema kwa vitendo vyao vyema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yûsuf alipofikia umri wa kukamilika nguvu za ujana wake, tulimpa fahamu na elimu. Na mfano wa malipo haya tuliyomlipa Yûsuf kwa wema wake, tutawalipa walio wema kwa wema wao. Katika haya kuna kumliwaza Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net