Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 21

Yusuf 12:21

يوسف

وَقَالَ ٱلَّذِى ٱشْتَرَىٰهُ مِن مِّصْرَ لِٱمْرَأَتِهِۦٓ أَكْرِمِى مَثْوَىٰهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوْ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُۥ مِن تَأْوِيلِ ٱلْأَحَادِيثِ ۚ وَٱللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰٓ أَمْرِهِۦ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Na yule aliyemnunua huko Misri alimwambia mkewe: "Mtengenezee huyu makazi ya heshima; huenda akatufaa au tukamfanya mwanetu." Basi hivyo ndivyo tulivyomuweka Yusuf imara katika ardhi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini wengi wa watu hawajui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makaazi ya hishima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu. Na kama hivyo tulimweka Yusuf katika nchi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui. [21]

[21] Yule aliye mnunua kule Misri alimwambia mkewe: Mfanyie wema huyu, na umhishimu, ili makao yake hapa nasi yawe mazuri. Huenda akatufaa, au tukamfanya kuwa ni mwenetu. Kama yalivyo kuwa makaazi yake ni mazuri na ya hishima, basi kadhaalika tulimjaalia Yusuf katika nchi ya Misri cheo kingine kikubwa, ili atekeleze uadilifu na mipango mizuri, na ili tumfunze kufasiri mambo na ndoto, ajue yatakayo kuwa kabla hayajwa, ili awe tayari kuyakabili! Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kutimiza kila jambo alitakalo. Kabisa haemewi na kitu. Lakini watu wengi hawajui siri ya hikima yake, na undani wa mipango yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wasafiri walipoondoka na Yûsuf kuelekea Misri, kiongozi wake alimnunua, naye ni waziri, na akamwambia mke wake, «Kaa naye vizuri na uyafanye mema makazi yake kwetu, huenda tukafaidika na utumishi wake, au tukamuweka hapa kwetu kama mtoto.» Na kama tulivyomuokoa Yûsuf na tukamfanya kiongozi wa Misri kuwa na huruma na yeye, vilevile tulimmakinisha kwenye ardhi ya Misri na tulimfanya asimamie hazina zake, na ili tumfundishe kufasiri ndoto na apate kujua matukio ya wakati unaokuja. Na Allah Mtukufu ni Mshindi kwa jambo Lake, uamuzi Wake ni wenye kupita, hakuna Mwenye kuutengua, lakini wengi sana kati ya watu hawajui kwamba mambo yote yako kwenye mkono wa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net