Yusuf 12:20
يوسفوَشَرَوْهُ بِثَمَنٍۭ بَخْسٍ دَرَٰهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا۟ فِيهِ مِنَ ٱلزَّٰهِدِينَ
Na wakamuuza kwa thamani duni, dirhamu za kuhesabika tu. Wala hawakuwa na haja naye.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
. Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa akali ya pesa. Wala hawakuwa na haja naye. [20]
[20] Wakamuuza Misri kwa bei ya chini kabisa, si kiasi chake! Thamani yake ilikuwa ni pesa chache tu! Wala hawakuwa wakimtakia Yusuf thamani kubwa, kwa kukhofia wasije watu wake wakamkuta wakamtambua, na wakawapokonya Yusuf.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ndugu zake wakamuuza kwa wachota maji miongoni mwa wasafiri kwa thamani chache ya dirhamu, na wakawa hawana haja na yeye, wanataka kuepukana na yeye. Hivyo ni kwa kuwa hawakijui cheo chake kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net