Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 19

Yusuf 12:19

يوسف

وَجَآءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا۟ وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُۥ ۖ قَالَ يَـٰبُشْرَىٰ هَـٰذَا غُلَـٰمٌ ۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَـٰعَةً ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِمَا يَعْمَلُونَ

Maana

Na ukaja msafara, kisha wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Hii ni bishara njema! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema hayo wanayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayo yatenda. [19]

[19] Wakaja watu upande ule wa kisima katika msafara wao wa kwendea Misri. Wakamtuma mtu kati yao wa kuchota maji kisimani awaletee. Akatumbukiza ndoo yake, akiivuta na Yusuf kang'ang'anilia! Yule mchota maji akapiga kelele za furaha: Kheri! Kheri gani hii na furaha! Huyu ni kijana! Wakamficha katika vitu vyao, wakamfanya ni bidhaa ya biashara! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka yote wayatendayo kwa ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Likaja kundi la wasafiri wakamtuma mwenye kuwatafutia maji, alipoiteremsha ndoo yake kisimani, Yûsuf aliishikilia. Hapo mchota maji alifurahi na akachangamka kwa kumuokota mtoto na akasema, «Ni bishara njema iliyoje! Huyu ni mtoto wa kiume mzuri.» Mchota maji na wenzake walimficha Yûsuf asijulikane na wasafiri wengine wasiwaoneshe, na wakasema, «Hii ni bidhaa tumeinunua.» Na Allah Mtukufu ni Mjuzi mno wa wanayomfanyia Yûsuf.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net