Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 18

Yusuf 12:18

يوسف

وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَٱللَّهُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ

Maana

Na walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakaja na kanzu yake ina damu ya uwongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza. [18]

[18] Wakaileta kanzu yake nayo ina damu, ati kuwa ni ushahidi wa yale madai yao ya kuwa ile ni damu ya Yusuf, apate kusadiki baba yao! Walakini yeye alisema: Hakika huyo mbwa mwitu hakumla kama mnavyo singizia, bali nafsi zenu zimekupelekeeni kufanya jambo kubwa, na mkalitimiza! Langu mimi ni kusubiri subira njema isiyo legalega kwa mliyo nikutisha. Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anaye takiwa msaada kwa huo upotovu mlio uzua na mnao udai.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakaja na kanzu yake ikiwa imerowa kwa damu ambayo si ya Yûsuf, ili iwe ni ushahidi juu ya ukweli wao, ikawa ni dalili ya urongo wao, kwa kuwa kanzu haikuchanika. Baba yao Ya‛qûb, amani imshukie, akawaambia, «Mambo sivyo kama mlivyosema, bali ni nafsi zenu zenye kuamrisha uovu ziliwapambia jambo ovu kumfanyia Yûsuf, mkaliona ni zuri na mkalifanya. Basi nitasubiri subira nzuri isiyokuwa na malalamishi kwa kiumbe chochote, na namuomba Allah Mtukufu msaada wa kuweza kuubeba huo urongo mnaoupanga; sitegemei uwezo wangu wala nguvu zangu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net