Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 17

Yusuf 12:17

يوسف

قَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَـٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئْبُ ۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَـٰدِقِينَ

Maana

Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapokuwa sisi ni wakweli.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli. [17]

[17] Wakasema: Ewe baba yetu! Sisi tulikwenda kushindana kupiga mishale na kwenda mbio, na tukamwacha Yusuf kwenye vitu vyetu avilinde. Mbwa mwitu akamla, na sisi tuko mbali tumeshughulika na mashindano! Na wewe hutusadiki tunayo yasema, ijapokuwa tunasema haki na kweli!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema, «Ewe baba yetu! Sisi tulikwenda tukawa tunashindana kukimbia na kurusha mishale, na tukamuacha Yûsuf kwenye vyombo vyetu na nguo zetu; na hatukufanya kasoro katika kumtunza, kwa kuwa tulimuacha mahali pa amani petu, na hatukumuacha isipokuwa kwa wakati mchache, mbwamwitu akamla. Na wewe hutatuamini, ingawa sisi ni wenye sifa ya ukweli, kwa sababu ya mapenzi yako makubwa kwa Yûsuf».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net