Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 26

Yusuf 12:26

يوسف

قَالَ هِىَ رَٰوَدَتْنِى عَن نَّفْسِى ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَآ إِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ

Maana

Yusuf akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za mwanamke akasema: Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo. [26]

[26] Yusuf akasema kujitetea: Ni yeye ndiye aliyenitaka, na akajaribu kunikhadaa! Ikawa ni kusutana. Alikata hukumu mmojapo katika jamaa zake mwenyewe yule mwanamke kwa kusema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi huyu bibi kasema kweli katika madai yake, na huyu kijana ni mwongo kwa aliyo yasema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yûsuf akasema, «Yeye ndiye aliyetaka hilo kwangu. Na akatoa ushahidi mtoto wa mlezini katika jamaa zake(mke wa kiongozi) na akasema, «Iwapo kanzu yake imepasuka kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli katika tuhma alizomfanyia na yeye (Yūsuf) ni miongoni mwa warongo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net