Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 96

Hud 11:96

هود

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَا وَسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ

Maana

Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi [96]

[96] Na hakika tulimtuma Musa na tukamuunga mkono kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na uthibitisho ulio wazi wenye nguvu juu ya nafsi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tulimtuma Mûsâ na dalili zetu za upweke wetu na hoja inayomfahamisha mwenye kuiona na kuitia akilini, kwa moyo wenye siha, kwamba zinatoa dalili ya upweke wa Allah Mtukufu na urongo wa kila anayedai umola asiyekuwa Yeye, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net