Hud 11:97
هودإِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَٱتَّبَعُوٓا۟ أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَآ أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ
Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao wakafuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uongofu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao walifuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uwongofu. [97]
[97] Tulimtuma ende kwa Firauni na wakuu katika watu wake. Firauni akamkanya Musa na akawaamrisha watu wake wamfuate yeye Firauni katika ukafiri wake. Wakenda kinyume na amri ya Musa! Wala amri ya Firauni haikuwa ni nyoofu yenye matokea mema hata istahiki kufuatwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tulimtuma Mûsã kwa Fir‛awn na wakubwa wa wafuasi wake na watukufu wa watu wake, Fir‛awn akakanusha na akawaamuru watu wake wamfuate yeye, wakamtii yeye na wakaenda kinyume cha amri ya Mûsã. Na hakuna uongofu wowote wala muongozo mwema katika amri ya Fir‛awn, ni ujinga mtupu, upotevu, ukanushaji na ujeuri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net