Hud 11:95
هودكَأَن لَّمْ يَغْنَوْا۟ فِيهَآ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ
Kama kwamba hawakuishi humo kwa ustawi. Zingatia ilivyoangamia Madyana, kama ilivyoangamia Thamud!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia walivyo angamia watu wa Madyana, kama walivyo angamia watu wa Thamud! [95]
[95] Mambo yakawishia, na athari zao zikapotea. Wakawa kama kwamba hawajapata kukaa katika majumba yao! Hali yao ikatamka ya kumzindua kila mwenye akili apate kuzingatia! Zingatia basi maangamizo ya Madyana, na vipi walivyo baidika na rehema ya Mwenyezi Mungu kama walivyo baidika watu wa Thamud kabla yao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kama kwamba wao hawakukaa kwenye nyumba zao wakati wowote. Jueni kwamba watu wa Madyan waliepushwa na rehema za Allah Mtukufu, kwa kuwa Allah Mtukufu aliwaangamiza watu wake na akawalaani, kama vile kina Thamûd walivyoepushwa na rehema Yake. Makabila mawili haya yalishirikiana katika kuwa mbali na rehema za Allah Mtukufu na kuangamia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net