Hud 11:94
هودوَلَمَّا جَآءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ٱلصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا۟ فِى دِيَـٰرِهِمْ جَـٰثِمِينَ
Na amri yetu ilipokuja, tulimwokoa sawasawa Shu'aibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na ukelele uliwanyakua wale waliodhulumu, na wakaishia wamekufa kifudifudi katika majumba yao!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na wakapambaukiwa majumbani mwao wamekufa kifudifudi! [94]
[94] Ilipo kuja amri yetu ya kuwaadhibu na kuwaangamiza, tulimwokoa Shua'ibu na walio amini pamoja naye wasipate adhabu na maangamizo. Kuokoka kwao kulikuwa kutokana na rehema iliyo tokana nasi. Ukelele uliwatwaa watu wa Madyana, na tetemeko la kuteketeza, wakapambaukiwa wamekwisha jifia katika majumba yao, wamelala kifudifudi, hawatukusiki hata kidogo!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na amri yetu ilipokuja ya kuwaangamiza watu wa Shu‛ayb, tulimuokoa mjumbe wetu Shu‛ayb na wale walioamini pamoja na yeye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu walipatwa na ukelele kutoka mbinguni ukawaangamiza na wakawa wako majumbani mwao wamepiga magoti wakiwa ni wafu hawatikisiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net