Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 93

Hud 11:93

هود

وَيَـٰقَوْمِ ٱعْمَلُوا۟ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّى عَـٰمِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَـٰذِبٌ ۖ وَٱرْتَقِبُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُمْ رَقِيبٌ

Maana

Na enyi kaumu yangu! Fanyieni katika mahali penu, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na ni nani mwongo. Na ngojeni, hakika mimi pia ninangoja pamoja nanyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu! Fanyeni mwezayo, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na nani aliye mwongo. Na ngojeni, mimi pia ninangoja pamoja nanyi. [93]

[93] Enyi watu wangu! Tendeni mnayo weza nyinyi kuyatenda. Kama hamsikilizi nasaha zangu, mimi naendelea kushikilia kutenda kinyume na vitendo vyenu. Na hapo tutakuja jua ni nani kati yetu ataye fikiwa na adhabu ya kumfedhehi na kumdhalilisha, na ni nani kati yetu ni mwongo - mimi ninaye kuonyeni na adhabu, au nyinyi mnao nionya kunifukuza katika mji wenu? Ngojeeni nini litatokea, na mimi nangojea pamoja nanyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu! Fanyeni mnaloliweza kwa njia yenu na namna yenu. Mimi ni mwenye kuendelea kufanya kwa njia yangu na nikitumia kile Allah Mtukufu Amenipa cha kuwalingania nyinyi kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu. Mtajua ni nani miongoni mwetu, itamjia adhabu yenye kumfanya mnyonge, na ni nani, miongoni mwetu, ni mrongo katika maneno yake: ni mimi au ni nyinyi? Na mngojee kitakachowashukia; mimi ni miongoni mwa wenye kungojea pamoja na nyinyi. Hili ni onyo kali kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net