Hud 11:92
هودقَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَهْطِىٓ أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذْتُمُوهُ وَرَآءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّى بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazingira yote mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda. [92]
[92] Akasema Shua'ibu: Enyi watu wangu! Hivyo jamaa zangu ndio wanastahiki kufanyiwa wema kuliko Mwenyezi Mungu. Wao mnawakumbuka, na mkataka kunifanyia jamala mimi kwa ajili yao. Lakini Yeye mmemsahau na mkamfanya kama kitu kilicho tupiliwa mbali nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola Mlezi wangu ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yafanya kwa kuyajua, hapana linalo fichikana kwake katika vitendo vyenu, na atakuhisabieni kwavyo hata ikiwa nyinyi mtasahau.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema, «Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni wenye nguvu zaidi na ni watukufu zaidi kwenu kuliko Allah Mtukufu? Na mumeitupa amri ya Mola wenu, mkaiweka nyuma ya migongo yenu, mkawa hamjilazimishi kufuata amri Zake na hamjiepushi na makatazo Yake. Hakika Mola wangu kwa mnayoyafanya Ameyazunguka, hakuna chochote katika matendo yenu kinafichika Kwake hata kama kina uzito wa chungu mdogo, na Atawalipa kwa hizo kwa haraka au baadaye».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net