Hud 11:91
هودقَالُوا۟ يَـٰشُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَـٰكَ ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ
Wakasema: Ewe Shu'aibu! Mengi katika hayo unayoyasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona dhaifu miongoni mwetu. Na lau kuwa si jamaa zako, tungekupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi katika hayo unayo yasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona huna nguvu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tunge kupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu. [91]
[91] Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi unayo yasema sisi hatuyafahamu! Na sisi tunakuhakikishia kuwa sisi tunakuona wewe dhaifu, huna nguvu zozote za kujitetea, wala kutukinaisha tukitaka kukutenda unayo yachukia. Na lau kuwa si kwa wema wetu kwa jamaa zako, kwani wao wanafuata dini yetu, tungeli kuulia mbali kwa kukupiga mawe. Na wewe si mtukufu kati yetu hata tukutukuze, na tukuhishimu, na tukukirimu na tuache kukuuwa kwa mawe! Ni wema tunao wafanyia jamaa zako tu ndio unao tuzuia tusikuuwe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walisema, «Ewe Shu‛ayb! Hatuyafahamu mengi unayotwambia, na sisi tunakuona wewe kuwa ni mnyonge kwetu, wewe si miongoni mwa watu wakubwa wala viongozi, na lau si kuwastahi jamaa zako tungalikuua kwa kukupiga mawe.»- Na kundi la jamaa zake lilikuwa ni katika watu wanaofuata mila yao.- «Na wewe huna cheo wala heshima katika nafsi zetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net