Hud 11:90
هودوَٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوٓا۟ إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّى رَحِيمٌ وَدُودٌ
Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu sana, Mwenye upendo mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu na Mwenye upendo. [90]
[90] Na mtakeni Mwenyezi Mungu akusameheni madhambi yenu, na rejeeni kwake kwa majuto mkiomba maghfira kila mtendapo dhambi. Hakika Mola wangu Mlezi ni mwingi wa rehema, ni mwenye mapenzi. Huwasamehe wenye kutubu, na anawapenda wenye kurejea kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ombeni kutoka kwa Mola wenu msamaha wa dhambi zenu, kisha rudini kumtii na endeleeni juu yake. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa rehema, ni Mwingi wa mapenzi na mahaba kwa aliyetubia na akarejea Kwake. Katika hii aya, pana kuthibitisha sifa ya raḥmah (kurehemu) na mawaddah (kupenda) kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kama inavyonasibiana na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net