Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 89

Hud 11:89

هود

وَيَـٰقَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِىٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَآ أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَـٰلِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم بِبَعِيدٍ

Maana

Na enyi kaumu yangu! Kuhalifiana nami kusiwapelekee hata mkasibiwa na mfano wa yale waliyosibiwa kaumu ya Nuhu, au kaumu ya Hud, au kaumu ya Saleh. Na kaumu ya Lut si mbali nanyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni hata mkasibiwa kama walivyo sibiwa watu wa Nuhu, au watu wa Hud, au watu wa Saleh. Na watu wa Lut' si mbali nanyi. [89]

[89] Na enyi watu! Hizi khitilafu ziliopo baina yangu na nyinyi zisikupelekeeni kufanya inda na mkashikilia ukafiri, hata yakakupateni yaliyo wapata kaumu ya Nuhu, na kaumu ya Huud, na kaumu ya Swaleh. Na wala zama na pahala pa kaumu Lut' na maangamizo yao si mbali nanyi! Basi zingatieni yasikusibuni yaliyo wasibu hao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Na enyi watu wangu, usiwapelekee uadui wenu kwangu na kunichukia na kuiacha Dini niliyonayo, kufanya ukakamavu na kuendelea na ukanushaji wa Allah Mtukufu mlionao. Kwani mkifanya hivyo, yatawapata nyinyi maangamivu kama yaliyowapata watu wa Nûh, au watu wa Hûd au watu wa S,ãlih,. Na hawakuwa watu wa Lût, na adhabu iliyowashukia ni mbali na nyinyi, si nchi waliyoishi wala zama walizokuwako».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net