Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 88

Hud 11:88

هود

قَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَءَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَرَزَقَنِى مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَآ أَنْهَىٰكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا ٱلْإِصْلَـٰحَ مَا ٱسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِىٓ إِلَّا بِٱللَّهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ

Maana

Akasema: Enyi kaumu yangu! Mnaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sitaki kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza. Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye ninarudi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea. [88]

[88] Yeye akasema: Enyi watu! Hebu nambieni, ikiwa mimi nina hoja iliyo wazi na ya yakini kutokana na Mola Mlezi wangu, naye akaniruzuku kwa fadhila yake riziki iliyo njema, je ingeli nifalia mimi nifiche aliyo niamrisha kukufikishieni, nako ni kuacha kuabudu masanamu, na kukutakeni mtimize vipimo na mizani, na muache kufanya uharibifu katika nchi? Na mimi si kama ninapenda kwenda kutenda haya ninayo kukatazeni, wala sitaki kwa mawaidha yangu, na nasaha zangu, na amri zangu, na makatazo yangu, ila kutengeneza kwa kadri ya ukomo wa uwezo wangu, na juhudi yangu, kama nilivyo jaaliwa. Wala sina uwezo wa kuifikilia haki ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kuungwa mkono naye, na ninamtegemea Yeye peke yake. Na kwake Yeye tu ndio ninarejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akasema Shu‛ayb, Enyi watu wangu, Mwaonaje iwapo mimi niko kwenye njia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu katika yale ninayowaitia ya kumtakasia Yeye ibada, na katika yale ninayowakataza ya kuharibu mali, na Akawa Ameniruzuku riziki ya ukunjufu ya halali iliyo nzuri? Na sitaki kuenda kinyume na nyinyi, nikafanya jambo nililowakataza; na sitaki, katika niwaamrishalo na niwakatazalo, isipokuwa ni kuwarekebisha kadiri ya uwezo wangu na kujimudu kwangu. Na kuafikiwa kwangu, katika kuipata haki na kujaribu kuwarekebisha, kuko kwa Allah Mtukufu. Kwake Yeye, Peke Yake, nimejitegemeza, na Kwake Yeye narejea kwa kutubia na kuelekea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net