Hud 11:87
هودقَالُوا۟ يَـٰشُعَيْبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِىٓ أَمْوَٰلِنَا مَا نَشَـٰٓؤُا۟ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلْحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ
Wakasema: Ewe Shu'aibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Ni swala zako ndizo zinazo kuamrisha tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu! [87]
[87] Wakasema kwa maskhara na kukejeli: Ewe Shua'ibu! Hivyo ni hizo swala zako ndizo zinazo kuamrisha kutushikilia tuache kuabudu masanamu waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu, na tuache kustarehe kutumia mali zetu kama tunavyoona wenyewe kuwa ni maslaha yetu? Hakika huo ndio mwisho wa upumbavu na utovu wa akili, wala haulingani na akili na rai njema tunazo kujua unazo; kwani wewe ni maarufu kwa ustahamilivu wako na uwongofu wako!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema, «Ewe Shu‛ayb, je swala hii ambayo unaendelea nayo ndiyo inayokuamuru wewe kwamba sisi tuache masanamu na mizimu ambayo baba zetu wanaabudu, au kwamba sisi tujizuie tusitumie njia tuziwezazo za hila na vitimbi katika kuchuma mali yetu?» Wakasema kwa njia ya kumcheza shere, «Wewe ndiye mwenye akili na hodari wa mipango ya usimamizi wa mali».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net