Hud 11:86
هودبَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ
Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ndivyo bora kwenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi si mlinzi wenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi siye mlinzi wenu. [86]
[86] Kidogo kinacho kuzidieni katika mali ya halali aliyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu ni bora kwenu kuliko chungu ya mali mnayo yakusanya kwa njia ya haramu, ikiwa nyinyi kweli mnamuamini Mwenyezi Mungu, na mnaepuka aliyo kukatazeni. Basi jipimeni nafsi zenu, na mumuangalie Mola wenu Mlezi. Mimi si mlinzi wenu wa kuchunga vitendo vyenu na kukupimieni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Kile kitakachosalia kwenu cha faida ya halali, baada ya kutimiza vipimo na mizani, kina baraka na ni chema kwenu kuliko kile mlichokua nacho cha pato la haramu kwa njia ya kupunja na mfano wake. Iwapo nyinyi mnamuamini Allah Mtukufu kikweli, basi fuateni amri Yake. Na mimi si mtunzi kwenu wa kuwahesabia matendo yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net