Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 85

Hud 11:85

هود

وَيَـٰقَوْمِ أَوْفُوا۟ ٱلْمِكْيَالَ وَٱلْمِيزَانَ بِٱلْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Maana

Na enyi kaumu yangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msienee katika ardhi mkifanya uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao; wala msieneze uovu katika nchi mkafanya uharibifu. [85]

[85] Enyi watu wangu! Toeni vipimo na mizani sawa na kwa uadilifu pale mnapo uza, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye ujeuri na fisadi katika nchi kwa kwiba mali ya watu na kupokonya, au kuvamia wapita njia, mkifanya fisadi ndio chumo la maisha yenu

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na enyi watu wangu, timizeni vipimo vya vibaba na mizani kwa usawa Wala msiwapunguzie watu haki zao katika jumla ya vitu vyao. Wala msiende katika ardhi mkifanya mambo ya kumuasi Allah Mtukufu na kueneza uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net